Jumapili, 29 Mei 2016
Ijumaa, 27 Mei 2016
Kivumbi Leo Uefa Champion League

Kuelekea katika Mchezo wa fainali ya League ya Mabingwa barani Ulaya zinazikutanisha Timu mbili kutoka katika jiji moja la Madrid na si wengine ni Atretico Madrid na Real Madrid, Timu ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa katika misimu mitatu mfululizo timu hizo zinazoongozwa na Makocha wawili ambao waliwahi kukupiga katika klabu hizo kipindi cha nyuma nawazungumzia Diego Simeone wa Atretico Madrid na Zinedine Zidane wa Real Madrid. Ikumbukwe kuwa Timu hizi mbili zilikutana kwa mara ya mwisho katika mashindano ya Uefa Champion League mawka 2013 na Real Madrid kuchukua ubingwa,Mchezo wa fainali wa Uefa Champion League utapigwa katika uwanja wa San Siro mjini Milan katika nchi ya Italia mchezo ambao utapigwa majira ya saa 3:45 kwa majira ya saa za Afrika Masharilki, timu hizo leo zimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo wa fainali. Kocha wa Atretico Madrid Diego Simeone akiwa katika mazungumzo ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho, anampongeza kocha wa Real Madrid kwa kufanikisha kusuka upya timu yake na kuifanya kuwa mpya na bora kwa muda mfupi tangu alipoichukua "Zidane amefanya kazi kubwa kukisuka kikosi cha Real Madrid kwa kipindi cha muda mfupi alichokaa na kikosi hicho, amefanya uamuzi mkubwa wa kumuamini na kumpa nafasi kiungo Casemiro, ameifanya timu nzima kuwa imara. Casemiro ndiye mchezaji muhimu kwasasa kwenye kikosi acha Real Madrid",hayo ni maneno ya Diego Simeone wakati anazungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa fainali ya klabu bingwa ulaya. Mshambuliaji wa Atretico Madrid Fernando Torres amesema, kuchukua taji la mabingwa Ulaya akiwa na Atretico itakuwa ni jambo jema licha ya kuwahi kutwaa taji hilo wakati akiwa na klabu ya Chelsea ya England. "Licha ya kushinda mataji kadhaa nikiwa na timu ya taifa ya Hispania pamoja na kutwaa taji la Uefa nikiwa na Chelsea mwaka 2012, nikishinda taji hili nikiwa na Atletico litakuwa muhimu sana kwenye maisha yangu",alisema Fernando Torres ambaye aliifungia Atletico bao pekee kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wakati Barca inaifunga Atletico kwa magoli 2-1 kwenye uwanja wa Camp Nou.
Jumatano, 25 Mei 2016
Twitter kufanyiwa mabadiliko ili kuwavutia watumiaji
Mtandao wa Twitter unafanyiwa marekebisho sheria zake ili kuwarahisishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo,zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika. Twiter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.Twiter imekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia, mwanzilishi mwenza wa Twiter na mkurugenzi mkuu Jack Dorsey,aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana. Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake. Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika mambo yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia. Brian Blau, ambaye ni mchambuzi kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo, Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao,Anaendelea kusema kuwa bado Twitter haijalishughulikia hilo.
Yanga Bingwa Kombe La FA

Timu ya Yanga Sports Club yenye maskani yake Jangwani jijini Dar es salaam yanyakuwa ubingwa wa kombe la FA dhidi ya wana Rambaramba wa Azam leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,mchezo uliotawaliwa kwa pasi nyingi sana na nguvu nyingi zaidi. Yanga ilikuwa ya kwanza kuona lango la Azam kupitia mshambuliaji wake Amisi Tambwe dakika ya 9 akiunganisha krosi safi kabisa ya Juma Abdul, mpaka dakika ya 18 hadi 20 kila timu inaonekana kushambulia kwa zamu lakini hakuna mashambulizi makali, dakika ya 22 bocco anajaribu kuingia vizuri kabisa lakini anaanguka mwenyewe na muamuzi anasema, goal kick. Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Yanga inaongoza goli 1-0, kipindi cha pili kinaanza kwa nguvu sana na mpaka dakika 47 Yanga wanafunga tena goli la 2 kupitia kwa mshambuliaji wake tena Amisi Tambwe anafunga bao safi kabisa katikati ya mabeki wa Azam Fc akiunganisha krosi Maridadi ya Simon Msuva, mnamo dakika ya 48 ya mchezo Azam Fc wanapata goli la kufutia machozi kupitia kwa Kavumbagu akiunganisha krosi safi ya Singano akitumia kifua kuukwamisha mpira wavuni. Mpaka dakika ya 79 ya mchezo hakuna timu iliyoona tena lango la timu nyingine lakini dakika ya 81 Deus Kaseke anawaamsha tena Mashabiki wa Yanga kwa kufunga goli safi kabisa akiunganisha krosi safi kabisa ya Simon Msuva na kuiandikia Yanga bao la 3 na matokeo kusomeka 3-0, mpaka dakika ya 90 zinakamilika zinaongezwa dakika 3, Yanga wanaonekana kucheza kwa taratibu sana kuonyesha kuwa wameridhika na mabao yao 3.
Mpira unamalizika kwa Yanga kuicharaza Azam mabao 3-1 na kuiwezesha Yanga kuwa Mabingwa wa kombe la shirikisho yani FA,
Jumanne, 24 Mei 2016
Igwe Fc kivumbi leo ligi ya Mabingwa Wa Mkoa

Ligi ya mabingwa wa Mkoa imeanza kutimua vumbi jana tarehe 23-05-2016 katika viwanja tofauti, Ambapo ligi hiyo inatarajiwa kuendelea leo katika viwanja tajwa,Ligi hiyo inayoshirikisha timu 27,imegawanywa katika makundi manne ambapo bingwa katika kila kundi atapanda dalaja hadi ligi daraja la pili msimu wa 2016-2017 ngazi ya taifa, kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza ligi dalaja la kwanza msimu wa 2017-2018. Timu ya Igwe Fc inatarajiwa kushuka dimbani leo kuikabili timu ya Mashujaa ya mkoa wa Kigoma,timu hizi zitamenyana vilivyo katika kiwanja cha Muleba mkoani kagera majira ya saa 10 za jioni ambapo katika kundi hilo kuna timu sita shiriki Geita Town Council Fc (Geita), Gold Sports Academy (Mwanza), Kabela city (Shinyanga), Ambassador Fc (Simiyu), Igwe Fc (Mara) na Mashujaa Fc (Kigoma). Timu ya igwe Fc yenye Maskani yake Mjini Musoma imeondoka na wachezaji thelathini pamoja na viongozi, akizungumza kocha mkuu wa Igwee Fc Bw.Sospeter alisema " Kikosi kimewasili salama hakuna mchezaji ambaye anaumwa tunamshukuru Mungu kwa hilo na tunachoweza kusema kuwa tumekuja kupambana na tutakuwa mabingwa wa kituo hiki". Pia kiongozi wa wachezaji (Captain) Mussa Issa alisema "Jambo la kwanza tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika salama safari ilikuwa ndefu sana,lakini kwa uwezo wake tumefika salama na kitu cha muhimu ni kupata matokeo katika kila hali ya kupambana katika kila mechi tutakayocheza".
Wachezaji ni Mussa Issa (Captain), Ramadhani Shabani (Resho) Hamisi Waziri (Bahanuzi) Evidence Charles, Anjero di Maria, Mpapi Nasibu (Bale) Gumbo Mfaume (Golikipa) Isihaka, Abraham,Bakari, Ramadhani Saidi (Kinusha), Ally Ramadhani (Gogo), Obadia, Shomary Shomary Kapombe(Kapombe), Willy Mnyambegu, Hashimu Kishikwambi, Devinyo Albinus, Edison Mtuli (Gamba), Majaliwa, God Muel, Samson Peter (Ndemla), Part, Rajabu (Golokipa), Edu White (White), Erasto Kabende,Mashaka, Frank, na Sajo Mwakalinga.
Jumatatu, 23 Mei 2016
Kampuni ya Mosan Limited inakutangazia nafasi za Kazi
- Osan COMPANY LIMITED INAKUTANGAZIA vacancies. Osan Company Limited inakutangazia positions kazikatika following areas (1): Officers marketing and sales (sales and marketing Officers) (2) Officials sales (sales officer) SIFA 1) Ability to run pikikpiki
2) The ability to sell and market, also add value to the business
3) Knowledge of the market
Send personal notes CV) on this Email
employment, Osan @ gmail.com.
Or this call for more information: +255717 49 87 73 The deadline for applications is May, 27,2016
Ijumaa, 20 Mei 2016
Rais Magufuli afuta uteuzi wa waziri Kitwanga
Habari zilizotufikia punde ni kuhusu maamuzi ya Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kuamua kutengua uteuzi wa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga. Rais Magufuli amemfuta waziri Kitwanga kutokana na waziri huyo kuingia bungeni kujibu swali linalohusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


