Jumatano, 31 Agosti 2016
Na:Fadhila Kizigo>>>Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro Laimarishwa
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limeimarisha viungo kwa kufanya mazoezi maeneo ya manispaa ya Morogoro. Akizungumza na waandishin wa habari kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Matei amesema kuwa mazoezi hayo yamelengwa kwa kuimarisha jeshi na si vinginevyo. Pia kamanda Matei amesema kuwa siku ya kesho wananchi wasiwe na hofu kwani jeshi letu limeimarishwa vyema kwa ulinzi hivyo maandamano hayo ni ya kichochezi hivyo ameomba wananchi kutokuwa na hofu kwani jeshi la polisi limeshakamata wale ambao ni wachochezi na wanaendelea kukamata kwa watakaoleta uchochezi wa maandamano.
Jumanne, 30 Agosti 2016
Na:Fadhila Kizigo>> Mh Kebwe Azindua Mashindano Ya Netball Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Steven Kebwe amezindua Rasmi mashindano ya Netball ligi dalaja la kwanza katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. Mashindano hayo yatakayofanyika viwanja vya Jamhuri mkoani humo yamezinduliwa kwa Mikoa mbalimbali kushiriki michuano hiyo. Hata hivyo Mh.Kebwe ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kuunga mkono suala la michezo kwani lipo kisheria na kufanya hivyo ni kujenga taifa la wanamichezo lakini pia Kebwe ameomba vijana kupambana na Ukimwi ili kujenga nguvu kazi ya Taifa.
Jumatatu, 29 Agosti 2016
>>>Serkali Yaifungia Magic Fm Na Radio 5
Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi. Hata hivyo Waziri Nape Nnauye amesema huku adhabu hiyo ikianza leo August 29 2016 pia ameiagiza kamati yake kuviita vyombo hivyo kwa ajili ya kuzungumza navyo kisha maamuzi mengine ya kisheria yatachukuliwa.
Jumapili, 28 Agosti 2016
Na:Fadhila Kizigo>>>Genk Wazidi Kung'ara Ubelgiji
Timu anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta imezidi kung'ara mara baada ya kuicharanga timu ya Zulte Waregem kwa goli 1-0 katika mchezo wa ligi ya Ubelgiji Zulta Waregem walikubali kichapo hicho wakiwa ugenini (Cristal Arena). Goli lililofungwa na Alejandlo Pozuelo dakika ya 80. Kwa mchezo huo Krc Genk inakamata nafasi ya tatu kati ya 16 kwenye msimamo wa ligi.
Tanzia:Deo Munish Afiwa Na Baba Yake Mzazi
Mlinda mlango nambari moja wa Yanga Deogratius Munish (Dida) amefiwa na baba yake mzazi leo mchana imeelezwa kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa wa facebook wa Naipenda Yanga bado chanzo cha kifo cha baba mzazi wa kipa huyo hakijawekwa wazi. Taarifa hiyo inaeleza hivi:"TANZIA..... Uongozi wa Yanga unasikitika kutangaza kifo cha baba yake na mlinda mlaango wetu deogratius munishi 'Dida', baba yake na dida amefariki leo mchana! Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi! Msiba utakuwa mikoroshini.Pumzika kwa amani mzee wetu.POLE SANA DEO MUNISH 'Dida' ". Hata hivyo katika mchezo wa leo Dida amecheza kwa umahiri mkubwa na kuisadia timu yake kupata clean sheet
Jumamosi, 27 Agosti 2016
Mch. Msigwa Atoa Kali Kuhusu Ukuta
Ni kuelekea katika Maandamano yaliyopewa jina la Ukuta yanayoratibiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ambapo yamepamgwa kuanza tarehe 1 ya mwezi wa 9 Aidha mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa (Chadema) ametoa kali mara baada ya kuandika katika kurasa yake ya
Twiter kuhusu Maandamano ya Ukuta Mch.Msigwa alisema kuwa "Mwanasiasa wa wa upinzani Tanzania kama anaogopa kukamatwa na Polisi ahamie CCM Huu ndio wakati wa kutofautisha BOYS FROM MEN".
Alhamisi, 25 Agosti 2016
Na.Fadhira Kizigo>>>Stand United Wakanusha Juu Ya Kujitoa VPL
Kufuatia kauli ya Waziri wa Michezo na Utamaduni Mh. Nape Nnauye juu ya sakata la Stand United kujitoa katika ligi ya Vodacom Tanzania bara kumekuwa na sintofahamu kwa mashabiki wa mpira nchini. Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi wa benchi la ufundi Stand United Muhibu Kano amemtaka Waziri Nape kuwaomba radhi watanzania kutokana na kitendo cha kutoa kauli hiyo kwan i angeitisha pande zote mbili kuzungumzia hilo na si kwa upande mmoja. Aidha Muhibu amesema amesema suala la kuanza kwa ligi vibaya kwa kutoka sare na Mbao Fc nikutokana na migogoro lakini chanzo cha migogoro ni wachezaji kukosa amani na kutofanya vizuri lakini wamejipanga vyema na mchezo unaofuata jumamosi 27 mwezi huu dhidi ya Kagera Sugar .
Jumatano, 24 Agosti 2016
Na. Fadhira Kizigo>>>>Yanga Out Shirikisho Kwa Point 4
Timu ya Yanga imemaliza michuano ya shirikisho Afrika dhidi ya Tp Mazembe kwa kukubali kipigo cha magori 3 kwa 1 Bolingi wa Tp Mazembe aliifungia timu yake gori la kwanza dakika ya 28, huku kipindi cha pili kuanza dakika 11 Rainford Kalaba aliifungia goli la pili Tp Mazembe kabla ya kuifungia goli la tatu mnamo dakika ya 64 huku goli la kufutia machozi kwa Yanga likiwekwa kimiani na Hamis Tambwe. Lakini kwa upande wa mashabiki wa mpira Mkoani
Morogoro Juma Demele alisema kuwa licha ya kushindwa naipongeza Yanga kwa kufanya vizuri hapo walipofika wana nafasi kwa mwakani kufanya vizuri zaidi hivyo kwa sasa wajipange kufanya vizuri kwa msimu huu wa ligi Tanzania bara pia Mohammed Mnyukwa alisema kuwa viongozi kuwa na ushirikiano na wachezajini jambo la kuzingatiwa kwenye klabu zetu nchini hivyo ni vyema kuwa umoja.
Ijumaa, 12 Agosti 2016
Na:Fadhira kizigo>>>Timu ya Polisi Morogoro Yatangaza kikosi chao
Timu ya polisi Morogoro yatambulisha kikosi chake kitakachoshiriki ligi daraja la kwanza hapo baadae mwezi huu, Afisa habari wa Polisi Morogoro Mwashibanda Shibanda amesema kuwa timu hiyo inamilikiwa na Wananchi na siyo jeshi la polisi hivyo anaomba mashirika mbalimbali kuiwezesha timu hiyo kwa fedha , vifaa,hata mawazo. Kashibanda alitaja orodha ya kikosi cha timu hiyo:walinda mlango. Benjamini Haule, Ramadhani Abedi, na Japhet Mwakyusa, walinzi wa kulia: Shabani Stambuli, Majid Msisis, walinzi wa kushoto: Saimon Samweli, Juma Ramadhani Haji: beki wa kati Omary Mtaki, Abrahaman Bakari, Omary Alawi na Godfrey Francis: viungo wa kati: Salum Bakari Nahodha, Juma Nade, James Ambrose, Bakari Mahadh na Abraham Thomas Bahufashi, winga wa kulia: Bantu Admin, David Christopher, na Hassan Kandabovu, winga wa kushoto: Nicholaus Kabipe, Fadhir Jamali, na Abdallah Maridodi, washambuliaji: Salum Kihimbwa, Ramadhani Kapela, Anyuerisa Mwaipora na Isaya Katua,
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)