Staa wa zamani wa vilabu vya Fc Barcelona na Chelsea Samuel Eto'o leo June 14 2016 amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Georgette Tra Lou, Eto'o amefunga ndoa na kuhudhuliwa na staa mwenzake wa Fc Barcelona Carlos Puyol na mkewe, Eto'o na mwenzake wamefunga ndoa leo Stezzano Italia.Jumanne, 14 Juni 2016
Etoo Afunga Ndoa Leo
Staa wa zamani wa vilabu vya Fc Barcelona na Chelsea Samuel Eto'o leo June 14 2016 amefunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Georgette Tra Lou, Eto'o amefunga ndoa na kuhudhuliwa na staa mwenzake wa Fc Barcelona Carlos Puyol na mkewe, Eto'o na mwenzake wamefunga ndoa leo Stezzano Italia.Ijumaa, 10 Juni 2016
Zoezi La Usajili Vitambulisho Vya Taifa Kukamilika Desemba 31 Mwaka Huu Nchi Nzima
Mamlaka ya usajili wa vitambulisho vya Taifa Nchini Tanzania (NIDA) wametangaza kuwa ifikapo tarehe 31 mwezi 12 mwaka huu usajili wa vitambulisho utakuwa umekamilika nchi nzima. Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam Bi.Rose Mdami, alisema "usajili utakamilika ifikapo tarehe 31 mwezi 12 mwaka huu Nchi zima na wananchi kuanza kutumia namba ya utambulisho kupata huduma" Bi.Rose Mdami ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hatiwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) aliwasisitiza Wananchi wote Nchini kuweza kujiandikisha mapema ili kuepuka usumbufu baadae. Pia Bi. Rose Mdami, amesema NIDA imepanga kutumia taarifa za NEC kukamilisha usajili wa awali na kutoa namba ya utambulisho kwa wananchi wote ambao hawakusajiliwa katika mfumo wa NIDA. Pia akifafanua, Bi.Rose amesema baada ya kuhakikisha kila mwananchi ana nambari ya Utambulisho.kila mwananchi atalazimika kukamilisha usajili wake ikiwa ni hatua ya kujaza vipengele vya maswali vilivyobakia katika fomu ya maombi ya vitambulisho kabla ya kupata utambulisho kamili. "Kama mnavyofahamu, katika usajili wa NEC fomu ilikuwa na vipengele 32 vya kujaza kulinganisha na fomu ya NIDA ambayo ina vipengele 74, hivyo ni lazima kila mwananchi kutambua, ili kuwa na utambulisho kamili lazima kujaza vipengele vilivyobaki pamoja na kuambatanisha nakala ya viambata vyake muhimu kuthibitisha taarifa za umri, uraia na makazi" alilisitiza.
Jumatano, 8 Juni 2016
Tff Yatoa Fomu Za Leseni Kwenye Vilabu

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za leseni za klabu (Club Licensing) za ligi ya vodacom Tanzania Bara (VPL) na zile za ligi daraja la kwanza ya Star Times. Klabu hizo zitatumiwa fomu hizo na kutakiwa kuzijaza na kuzirejesha kabla ya June 19, mwaka huu ikiwa ni siku 10 mara baada ya Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) kuwatumia fomu hizo. Klabu itakayojaza fomu hizo kwa wakati ndiyo ambayo maombi yake ya leseni yatashughulikiwa mapema. Tayari TFF imeteua kamati ya leseni ya klabu (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi daraja la Kwanza na kutoa uamuzi wa kuzikubali au kuzikataa kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya klabu. Wajumbe walioteuliwa kwenye kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof.Mshindo Msolla. Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi ya Vodacom na Ligi daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016-2017. Kwa Klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (Sporting) viwanja (infrasructure), utawala (administrate and personal), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapata leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi. Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, z itakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3)ya kanuni ya leseni ya klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo itakayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa kamati ya leseni ya TFF.
Alhamisi, 2 Juni 2016
Zengwe Laibuka Upinzani Na Spika Bungeni

June 02 2016 Kambi rasmi ya upinzani bungeni imekutana na waandishi wa habari Dodoma ili kuwasilisha mambo makuu sita imetoa sababu kuu sita za kutaka Naibu spika wa Tanzania Dr.Tulia Ackson aondolewe madarakani kwa azimio la kuvunja sheria inayoendesha bunge. Akiongea kwa niaba ya kambi ya upinzani mbunge wa Simanjiro James Millya amesema "Naibu spika Tulia Ackson ameweka maslahi ya chama chake cha siasa mbele kuliko maslahi ya bunge kinyume na kanuni ya 8 (b) ya kanuni za kudumu za bunge" "kutoa uamuzi wa mwongozo ambao ulikuwa unakiuka katiba isemayo kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake muongozo uliokuwa unapinga udhalilishaji wa wabunge Wanawake UKAWA kwamba hawapati Ubunge mpaka waitwe baby, muongozo ulioombwa Dr.Tulia aliudharau" Tarehe 30 May Naibu spika huyo huyo aliamua kwa makusudi kuvunja ibara ya katiba ya Jamhuli ya muungano wa Tanzania kumzuia Mh. Joshua Nassari kutimiza majukumu yake ya kikatiba ya kusimamia na kuishauri serikali, ni pale alipoomba muongozo wa jambo la dharura la kufukuzwa kwa Wanachuo wa UDOM, Dr. Tulia alisema hoja hiyo sio ya dharura na wala haikuwa na haja yoyoteya kuwasilishwa. Kitendo cha naibu spika Dr. Tulia kukataa taarifa tofauti iliyowasilishwa na Wabunge wanne wa upinzani ambao ni wajumbe wa kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge jambo ambalo ni kinyume cha kanuni ya tano ambapo maamuzi yake haya yalisaidia kuwafukuza wabunge saba wanaolitumikia taifa hili, adhabu iliyotolewa haikuwa adhabu inayostahili.
Jumapili, 29 Mei 2016
TTCL Yazindua Nembo Mpya na 4G LTE
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) yazindua Nembo mpya pamoja na kuzindua huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE Leo jijini Dar es salaam.kampuni hiyo imefanya mabadiliko makubwa ya nembo yake pamoja kuzindua huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE ikiwa ni muendelezo wa mpango wa kufanya mabadiliko ya kibiashara kwa kampuni hiyo. Nembo hiyo mpya ya TTCL na huduma ya 4G LTE vimezinduliwa leo jijini Dar es salaam na waziri wa Ujenzi Uchukuzi, na Mawasiliano,ProfesaMakame Mbarawa huku akiipongeza kwa hatua ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji na uwajibikaji unaolenga kuonesha tija na ubora. Waziri Mbarawa alisema uzinduzi huo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli la kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu, na kufikia viwango vya juu kabisa vya kutoa huduma kwa umma sambamba na mpango mkakati wa TTCL, kibiashara kwa kipindi cha mwaka 2016-2018. "Pamoja na pongezi hizi za dhati, naomba mtambue kuwa uzinduzi huu hautakuwa na maana yoyote pasipo mabaliko ya kiutendaji utoaji huduma kwa wateja. Watumiaji wa huduma zenu wanahitaji mabadiliko ya dhati ya viwango vya huduma na utendaji ili kuwajengea imani juu ya uwezo wenu wa kuwahudumia," alisema Waziri Mbarawa, Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema uzinduzi wa nemnbo mpya ya TTCL, unaleta muonekano mpya wa kampuni unaoenda sambamba na mageuzi ambayo yanaendelea katika kuboresha miundombinu ya mtandao wa simu data. Alisema katika safari ya mageuzi TTCL imefanikiwa kuboresha miundombinu ya simu za mezani na mkononi kwa kuleta teknolojia ya 2G, GSM, 3G, UMTS, na LTE Sokoni ili kwenda sambamba na ushindani wa soko la mawasiliano. "Teknolojia hizi zitaisaidia kuongeza ufanisi, ubunifu katika kutoa huduma ya simu za mezani, simu za mkononi na huduma ya intaneti zenye ubora wa hali ya juu ya uhakika na gharama nafuu,"alisema Dk. Kazaura. Alisema kwa sasa kampuni hiyo inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya data nchi nzima, hali ambayo itaongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wetu wote ndani na nje ya nchi.
Ijumaa, 27 Mei 2016
Kivumbi Leo Uefa Champion League

Kuelekea katika Mchezo wa fainali ya League ya Mabingwa barani Ulaya zinazikutanisha Timu mbili kutoka katika jiji moja la Madrid na si wengine ni Atretico Madrid na Real Madrid, Timu ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa katika misimu mitatu mfululizo timu hizo zinazoongozwa na Makocha wawili ambao waliwahi kukupiga katika klabu hizo kipindi cha nyuma nawazungumzia Diego Simeone wa Atretico Madrid na Zinedine Zidane wa Real Madrid. Ikumbukwe kuwa Timu hizi mbili zilikutana kwa mara ya mwisho katika mashindano ya Uefa Champion League mawka 2013 na Real Madrid kuchukua ubingwa,Mchezo wa fainali wa Uefa Champion League utapigwa katika uwanja wa San Siro mjini Milan katika nchi ya Italia mchezo ambao utapigwa majira ya saa 3:45 kwa majira ya saa za Afrika Masharilki, timu hizo leo zimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo wa fainali. Kocha wa Atretico Madrid Diego Simeone akiwa katika mazungumzo ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho, anampongeza kocha wa Real Madrid kwa kufanikisha kusuka upya timu yake na kuifanya kuwa mpya na bora kwa muda mfupi tangu alipoichukua "Zidane amefanya kazi kubwa kukisuka kikosi cha Real Madrid kwa kipindi cha muda mfupi alichokaa na kikosi hicho, amefanya uamuzi mkubwa wa kumuamini na kumpa nafasi kiungo Casemiro, ameifanya timu nzima kuwa imara. Casemiro ndiye mchezaji muhimu kwasasa kwenye kikosi acha Real Madrid",hayo ni maneno ya Diego Simeone wakati anazungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa fainali ya klabu bingwa ulaya. Mshambuliaji wa Atretico Madrid Fernando Torres amesema, kuchukua taji la mabingwa Ulaya akiwa na Atretico itakuwa ni jambo jema licha ya kuwahi kutwaa taji hilo wakati akiwa na klabu ya Chelsea ya England. "Licha ya kushinda mataji kadhaa nikiwa na timu ya taifa ya Hispania pamoja na kutwaa taji la Uefa nikiwa na Chelsea mwaka 2012, nikishinda taji hili nikiwa na Atletico litakuwa muhimu sana kwenye maisha yangu",alisema Fernando Torres ambaye aliifungia Atletico bao pekee kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wakati Barca inaifunga Atletico kwa magoli 2-1 kwenye uwanja wa Camp Nou.
Jumatano, 25 Mei 2016
Twitter kufanyiwa mabadiliko ili kuwavutia watumiaji
Mtandao wa Twitter unafanyiwa marekebisho sheria zake ili kuwarahisishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo,zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika. Twiter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.Twiter imekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia, mwanzilishi mwenza wa Twiter na mkurugenzi mkuu Jack Dorsey,aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana. Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake. Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika mambo yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia. Brian Blau, ambaye ni mchambuzi kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo, Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao,Anaendelea kusema kuwa bado Twitter haijalishughulikia hilo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)


