Jumapili, 29 Mei 2016
Ijumaa, 27 Mei 2016
Kivumbi Leo Uefa Champion League
Kuelekea katika Mchezo wa fainali ya League ya Mabingwa barani Ulaya zinazikutanisha Timu mbili kutoka katika jiji moja la Madrid na si wengine ni Atretico Madrid na Real Madrid, Timu ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa katika misimu mitatu mfululizo timu hizo zinazoongozwa na Makocha wawili ambao waliwahi kukupiga katika klabu hizo kipindi cha nyuma nawazungumzia Diego Simeone wa Atretico Madrid na Zinedine Zidane wa Real Madrid. Ikumbukwe kuwa Timu hizi mbili zilikutana kwa mara ya mwisho katika mashindano ya Uefa Champion League mawka 2013 na Real Madrid kuchukua ubingwa,Mchezo wa fainali wa Uefa Champion League utapigwa katika uwanja wa San Siro mjini Milan katika nchi ya Italia mchezo ambao utapigwa majira ya saa 3:45 kwa majira ya saa za Afrika Masharilki, timu hizo leo zimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo wa fainali. Kocha wa Atretico Madrid Diego Simeone akiwa katika mazungumzo ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho, anampongeza kocha wa Real Madrid kwa kufanikisha kusuka upya timu yake na kuifanya kuwa mpya na bora kwa muda mfupi tangu alipoichukua "Zidane amefanya kazi kubwa kukisuka kikosi cha Real Madrid kwa kipindi cha muda mfupi alichokaa na kikosi hicho, amefanya uamuzi mkubwa wa kumuamini na kumpa nafasi kiungo Casemiro, ameifanya timu nzima kuwa imara. Casemiro ndiye mchezaji muhimu kwasasa kwenye kikosi acha Real Madrid",hayo ni maneno ya Diego Simeone wakati anazungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa fainali ya klabu bingwa ulaya. Mshambuliaji wa Atretico Madrid Fernando Torres amesema, kuchukua taji la mabingwa Ulaya akiwa na Atretico itakuwa ni jambo jema licha ya kuwahi kutwaa taji hilo wakati akiwa na klabu ya Chelsea ya England. "Licha ya kushinda mataji kadhaa nikiwa na timu ya taifa ya Hispania pamoja na kutwaa taji la Uefa nikiwa na Chelsea mwaka 2012, nikishinda taji hili nikiwa na Atletico litakuwa muhimu sana kwenye maisha yangu",alisema Fernando Torres ambaye aliifungia Atletico bao pekee kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wakati Barca inaifunga Atletico kwa magoli 2-1 kwenye uwanja wa Camp Nou.
Jumatano, 25 Mei 2016
Twitter kufanyiwa mabadiliko ili kuwavutia watumiaji
Mtandao wa Twitter unafanyiwa marekebisho sheria zake ili kuwarahisishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo,zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika. Twiter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.Twiter imekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia, mwanzilishi mwenza wa Twiter na mkurugenzi mkuu Jack Dorsey,aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana. Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake. Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika mambo yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia. Brian Blau, ambaye ni mchambuzi kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo, Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao,Anaendelea kusema kuwa bado Twitter haijalishughulikia hilo.
Yanga Bingwa Kombe La FA
Timu ya Yanga Sports Club yenye maskani yake Jangwani jijini Dar es salaam yanyakuwa ubingwa wa kombe la FA dhidi ya wana Rambaramba wa Azam leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,mchezo uliotawaliwa kwa pasi nyingi sana na nguvu nyingi zaidi. Yanga ilikuwa ya kwanza kuona lango la Azam kupitia mshambuliaji wake Amisi Tambwe dakika ya 9 akiunganisha krosi safi kabisa ya Juma Abdul, mpaka dakika ya 18 hadi 20 kila timu inaonekana kushambulia kwa zamu lakini hakuna mashambulizi makali, dakika ya 22 bocco anajaribu kuingia vizuri kabisa lakini anaanguka mwenyewe na muamuzi anasema, goal kick. Mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Yanga inaongoza goli 1-0, kipindi cha pili kinaanza kwa nguvu sana na mpaka dakika 47 Yanga wanafunga tena goli la 2 kupitia kwa mshambuliaji wake tena Amisi Tambwe anafunga bao safi kabisa katikati ya mabeki wa Azam Fc akiunganisha krosi Maridadi ya Simon Msuva, mnamo dakika ya 48 ya mchezo Azam Fc wanapata goli la kufutia machozi kupitia kwa Kavumbagu akiunganisha krosi safi ya Singano akitumia kifua kuukwamisha mpira wavuni. Mpaka dakika ya 79 ya mchezo hakuna timu iliyoona tena lango la timu nyingine lakini dakika ya 81 Deus Kaseke anawaamsha tena Mashabiki wa Yanga kwa kufunga goli safi kabisa akiunganisha krosi safi kabisa ya Simon Msuva na kuiandikia Yanga bao la 3 na matokeo kusomeka 3-0, mpaka dakika ya 90 zinakamilika zinaongezwa dakika 3, Yanga wanaonekana kucheza kwa taratibu sana kuonyesha kuwa wameridhika na mabao yao 3.
Mpira unamalizika kwa Yanga kuicharaza Azam mabao 3-1 na kuiwezesha Yanga kuwa Mabingwa wa kombe la shirikisho yani FA,
Jumanne, 24 Mei 2016
Igwe Fc kivumbi leo ligi ya Mabingwa Wa Mkoa
Ligi ya mabingwa wa Mkoa imeanza kutimua vumbi jana tarehe 23-05-2016 katika viwanja tofauti, Ambapo ligi hiyo inatarajiwa kuendelea leo katika viwanja tajwa,Ligi hiyo inayoshirikisha timu 27,imegawanywa katika makundi manne ambapo bingwa katika kila kundi atapanda dalaja hadi ligi daraja la pili msimu wa 2016-2017 ngazi ya taifa, kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza ligi dalaja la kwanza msimu wa 2017-2018. Timu ya Igwe Fc inatarajiwa kushuka dimbani leo kuikabili timu ya Mashujaa ya mkoa wa Kigoma,timu hizi zitamenyana vilivyo katika kiwanja cha Muleba mkoani kagera majira ya saa 10 za jioni ambapo katika kundi hilo kuna timu sita shiriki Geita Town Council Fc (Geita), Gold Sports Academy (Mwanza), Kabela city (Shinyanga), Ambassador Fc (Simiyu), Igwe Fc (Mara) na Mashujaa Fc (Kigoma). Timu ya igwe Fc yenye Maskani yake Mjini Musoma imeondoka na wachezaji thelathini pamoja na viongozi, akizungumza kocha mkuu wa Igwee Fc Bw.Sospeter alisema " Kikosi kimewasili salama hakuna mchezaji ambaye anaumwa tunamshukuru Mungu kwa hilo na tunachoweza kusema kuwa tumekuja kupambana na tutakuwa mabingwa wa kituo hiki". Pia kiongozi wa wachezaji (Captain) Mussa Issa alisema "Jambo la kwanza tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika salama safari ilikuwa ndefu sana,lakini kwa uwezo wake tumefika salama na kitu cha muhimu ni kupata matokeo katika kila hali ya kupambana katika kila mechi tutakayocheza".
Wachezaji ni Mussa Issa (Captain), Ramadhani Shabani (Resho) Hamisi Waziri (Bahanuzi) Evidence Charles, Anjero di Maria, Mpapi Nasibu (Bale) Gumbo Mfaume (Golikipa) Isihaka, Abraham,Bakari, Ramadhani Saidi (Kinusha), Ally Ramadhani (Gogo), Obadia, Shomary Shomary Kapombe(Kapombe), Willy Mnyambegu, Hashimu Kishikwambi, Devinyo Albinus, Edison Mtuli (Gamba), Majaliwa, God Muel, Samson Peter (Ndemla), Part, Rajabu (Golokipa), Edu White (White), Erasto Kabende,Mashaka, Frank, na Sajo Mwakalinga.
Jumatatu, 23 Mei 2016
Kampuni ya Mosan Limited inakutangazia nafasi za Kazi
- Osan COMPANY LIMITED INAKUTANGAZIA vacancies. Osan Company Limited inakutangazia positions kazikatika following areas (1): Officers marketing and sales (sales and marketing Officers) (2) Officials sales (sales officer) SIFA 1) Ability to run pikikpiki
2) The ability to sell and market, also add value to the business
3) Knowledge of the market
Send personal notes CV) on this Email
employment, Osan @ gmail.com.
Or this call for more information: +255717 49 87 73 The deadline for applications is May, 27,2016
Ijumaa, 20 Mei 2016
Rais Magufuli afuta uteuzi wa waziri Kitwanga
Habari zilizotufikia punde ni kuhusu maamuzi ya Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kuamua kutengua uteuzi wa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Charles Kitwanga. Rais Magufuli amemfuta waziri Kitwanga kutokana na waziri huyo kuingia bungeni kujibu swali linalohusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa
Alhamisi, 19 Mei 2016
Manny Pacquiao Useneta Filipino
Bondia mwenye jina kubwa katika ulimwengu wa ngumi Manny Pacquiao may 19 2016 amengia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kushinda nafasi ya useneta katika bunge nyumbani kwao Filipino,Pacquiao amefanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kura milioni 16, Pacquiao anakuwa ni miongoni mwa watu 12 waliofanikiwa kushinda nafasi ya seneta katika bunge la Filipino,ushindi wa bondia huyo maarufu unatoa tafsiri huenda siku akapata nafasi ya kugombea nafasi za juu za uongozi wa nchi hiyo hususani Rais. Kama utakumbuka vizuri Manny Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 amefanikiwa kushinda mataji kadhaa ya ubingwa wa ngumi, Pacquiao ndio bondia aliyepigana na Mayweather na kupoteza kwa point katika pambano linalotajwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.
Aitel Money yazindua kampeni ya mr money kwa wateja wake
Managing Director of Airtel Sunil Collasso Lord speaking while tagging Mr Money that ensures customer service users of Airtel Money reliable and cost-effective in financial services. Airtel Tanzania introduces "Mr Money" friend and gave the good news will help customers solve their challenges and educate them about the various benefits provided through the services of Airtel Money. Mr Money has been made to show the diversity in financial services and eliminate layers in the services we provide to market and make them the same.
mwanasheria mkuu wa serikali atoa neno juu ya mawakili
Mwanasheria mkuu wa serikali mh.George Masaju amewataka Mawakili wa serikali kuwa makini na kutoa ushauri kwa uadilifu na uweledi wa hali ya juu pindi wanapotoa ushauri wa kisheria kuhusu mikataba mbalimbali.Mhe. Masaju ameitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na mawakili wa serikali wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanayohusu uhakiki wa mikataba ya ununuzi wa umma leo mjini dodoma.Alisema ni vyema wakatekeleza jukumu hilo kwa makini kwani ushauri unaotolewa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kupitia mawakili hao ndio msimamo wa serikali."Ninapenda kuwakumbusha kwamba ninyi ni watumishi wa umma na mnaongozwa na sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 pamoja na kanunui zake za mwaka 2003"aalisema Mhe.Masaju na kuongeza kuwa: "kama walivyo watumishi wa wengine wa umma na kwa msingi huu,ninyi ni sehemu ya serikali na nafasi yenu katika serikali ni kubwa".pia aliwataka wanasheria wa serikali kujengewa uwezo kuhusu uhakiki wa mikataba na iwapo watashindwa kutekeleza wajibu huo ipasavyo watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu.
Jumatano, 18 Mei 2016
liverpool yapigwa fainali ya europa league
Timu ya liverpool ya england imejikuta ikipigwa kichapo kikali kutoka kwa waspain wa sevilla \wakishuhudia timu hiyo ikichukua ubingwa wa europa league aa kukatisha ndoto za liverpool kushiriki mashindano ya uefa hapo mwakani.,timu hiyo ambayo inanolewa na kocha mkongwe Jurgen Klopp ilianza kujipatia goli kupitia mshambuliaji wao Danny Sturrige hadi kipimdi cha kwanza kinamalizika liverpool ilikuwa inaogoza kwa bao moja, ingwe ya pili ya mchezo ilianza kwa kasi sana na mnamo dakika ya 46 vijana wa sevilla walipata gori la kusawazisha goli lililofungwa na Gameiro akimalizia pasi safi kutoka kwa Mariano,Magoli mengine mawili yaliwekwa kimiani na Coke dakika ya 64 na 70, Na mchezo ukimalizika kwa mabao 3-1 na vijana wa kocha Unai Emery kujinyakulia ubingwa huo katika
kiwanja cha st.jacob pack dubai.
Jumanne, 17 Mei 2016
Utafiti umefanyika Tanzania imetajwa katika list za juu za nchi zisizokuwa waaminifu
- utafiti umefanywa na wanafunzi wa university of Nottingham uingereza ukihusisha nchi 159,wanafunzi wa chuo kikuu cha Nottingham wamefanya utafiti wa kugundua ni nchi zipi zinazoongoza kwa uaminifu au ukweli duniani,wanafunzi hao wamefanya tafiti huku wakichanganya na data za 2013 za ukwepaji wa kodi ,rushwa na udanganyifu katika siasa lakini wamegundua kuwa nchi za Lithunian, Uholanzi,Uingereza,Sweden,Ujerumani,na Italia zimetajwa katika list ya nchi zinazoongoza kwa uaminifu.Wakati nchi za Tanzania,China,Uturuki,Poland,na Morocco zimetajwa kuwa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza watu wake kutokuwa waaminifu,utafiti huo unaelezea kuwa watu wanaoishi katika nchi zenye rushwa na siasa za udanganyifu wamekuwa sio waaminifu au wakweli,wakati watu wanaotokea katika nchi ambazo hazina rushwa na ukwepaji kodi ni waaminifu.
Jumatatu, 16 Mei 2016
))))) waziri mkuu azumngumzia suala zima la kutokurusha moja kwa moja matangazo ya bunge
Waziri mkuu kassim majaliwa azumngumzia suala la kutorusha kwa matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni kuwa kutokufanya hivyo kutapunguza gharama na kuokoa fedha zinazopotea bila sababu na kwa kufanya hivyo ni kuendeleza kauli mbiu ya hapa kazi tu! pia alisema kutokana na suala hilo kutawafanya watanzania kufanya kazi kuliko kutumia muda mwingi kuangalia bunge na badala yake bunge litakuwa linarushwa usiku.
Jumapili, 15 Mei 2016
Wema Sepetu afunguwa kampuni mpya ya lipsstick
RAIS JPM AENDELEZA GURUDUMU
)))))) New information continues to seek president John Magufuri sugar in Every corner: complete information click the links below
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)