Mwanasheria mkuu wa serikali mh.George Masaju amewataka Mawakili wa serikali kuwa makini na kutoa ushauri kwa uadilifu na uweledi wa hali ya juu pindi wanapotoa ushauri wa kisheria kuhusu mikataba mbalimbali.Mhe. Masaju ameitoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na mawakili wa serikali wakati wa ufunguzi wa mafunzo yanayohusu uhakiki wa mikataba ya ununuzi wa umma leo mjini dodoma.Alisema ni vyema wakatekeleza jukumu hilo kwa makini kwani ushauri unaotolewa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kupitia mawakili hao ndio msimamo wa serikali."Ninapenda kuwakumbusha kwamba ninyi ni watumishi wa umma na mnaongozwa na sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 pamoja na kanunui zake za mwaka 2003"aalisema Mhe.Masaju na kuongeza kuwa: "kama walivyo watumishi wa wengine wa umma na kwa msingi huu,ninyi ni sehemu ya serikali na nafasi yenu katika serikali ni kubwa".pia aliwataka wanasheria wa serikali kujengewa uwezo kuhusu uhakiki wa mikataba na iwapo watashindwa kutekeleza wajibu huo ipasavyo watawajibishwa kwa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni