Alhamisi, 19 Mei 2016

Manny Pacquiao Useneta Filipino

Bondia mwenye jina kubwa katika ulimwengu wa ngumi Manny Pacquiao may   19   2016   amengia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kushinda nafasi ya useneta katika bunge nyumbani kwao Filipino,Pacquiao amefanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kura milioni 16, Pacquiao anakuwa ni miongoni mwa watu 12 waliofanikiwa kushinda nafasi ya seneta katika bunge la Filipino,ushindi wa bondia huyo maarufu unatoa tafsiri huenda siku akapata nafasi ya kugombea nafasi za juu za uongozi wa nchi hiyo hususani Rais. Kama utakumbuka vizuri Manny Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 amefanikiwa kushinda mataji kadhaa ya ubingwa wa ngumi, Pacquiao ndio bondia aliyepigana na Mayweather na kupoteza kwa point katika pambano linalotajwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni