Alhamisi, 30 Juni 2016

Kubenea na Joseph Mbilinyi Wasimamishwa kuhudhuria bungeni.


Mbunge wa Ubungo Chadema amesimamishwa  kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT  Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli.                                                                                                                                                                                               Pia Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph  Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo june 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge  baada ya kukiri mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili naye achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni