Mshambuliaji wa Taifa Stars,Elius Maguli amekamilisha usajili wake kutoka Stand United ya Shinyanga kama mchezaji huru na kujiunga katika klabu ya Dhofar Sc ya Oman Proffessional League. Elius Maguli amejiunga na klabu hiyo ya Oman baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Stand United ya Shinyanga Maguli anajiunga na timu hiyo ambayo imemaliza katika nafasi ya tano ligi ya kulipwa mwaka mmoja uliopita ni hatua kubwa kwa kijana mdogo kama Maguli ambaye ameondoka VPL akiwa amefunga jumla ya magoli 33 katika misimu yake mitatu aliyocheza kama mchezaji wa vilabu vya Shooting, Simba, na Stand United. Pia Maguli ni mshambuliajiwa kikiosi cha kwanza katika timu ya Taifa ya Tanzania kwa mwaka mmoja sasa akicheza sambamba na Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta katika safu ya mashambulizi kwa maana hiyo, kocha Charles Mkwasa ataendelea kufurahia vijana wake watatu wakiwa ng'ambo ya nchi kuendeleza vipaji vyao na kudumisha vipaji vyao na kudumisha viwango vyao vya kiuchezaji. Dhofar ni timu iliyoanzishwa miaka 44 iliyopita, na Oman kuna mishahara mikubwa hadi kufikia dora 30,000 kwa mchezaji wa kiwango cha Maguli. Mchezaji wa kikosi cha kwanza wa timu ya taifa. sasa mastaa watatu wa Stars katika kikosi cha mashambulizi wapo ng'ambo. kila la heri Elius Maguli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni