Alhamisi, 27 Oktoba 2016
Jumatano, 14 Septemba 2016
Na:Fadhila Kizigo>>>Jeshi La Polisi Mkoani Morogoro Lakamata Silaha
Jeshi la polisi Mkoani Morogoro limeendelea na msako wa silaha kwa watu ambao wanamiliki kinyume na sheria ambapo katika msako huo Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG ikiwa na magazine moja ikiwa na risasi nyingine 39 zikihifadhiwa katika mfuko wa naironi, zikiwemo risasi 2 za bunduki aina ya Rifle. Hata hivyo kufuatia tukio hilo mtuhumiwa mmoja aitwaye God s/o Octavian, 44 mkazi wa mkundi, anashikiliwa na Polisi kwa kupatikana na silaha hiyo. Aidha katika tukio lingine polisi mkoani Morogoro linamshilia Anna d/o Lumbano, 33 mkazi wa dsm kwa tuhuma za wizi wa mtoto Angel d/o Meck, mwenye umri wa siku kumi, akiwa anamtorosha kuelekea Dar es salaam Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Ijumaa, 9 Septemba 2016
Na:Fadhila Kizigo Bangi Zakamatwa Morogoro
Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watu 4 kwa kukutwa na Bangi zaidi ya kg 50. Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani Morogoro Ulrich Matei amesema kuwa mnamo tarehe 8/9/2016 majira ya saa tano asubuhi maeneo ya kasanga Morogoro waliwakamata watu wanne waliokuwa na mzigo wa bangi. Aidha Kamanda Matei amesema kuwa askari wakiwa doria walifanikiwa kuwakamata Rehema Omary mkazi wa Kasanga, Mbega Hassan, Abuubakari Salum na Chiku Omary wote wakazi wa mji mpya wakiwa na viroba viwili vya bangi na mfuko wa rambo mweusi vilivyohifadhiwa nyumbani kwa Rehema Omary kwaajili ya kusafirishwa.Hata hivyo kamanda Matei amesema kuwa watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na hatua za kufikishwa mahakamani zinafuata.
Lwakatale Alipia Faini Wafungwa 50
Mchungaji Lwakatale amewalipia zaidi ya wafungwa 50 waliokuwa wamehukumiwa kwenda jela kwa kushindwa kulipia faini za kiwango tofauti tofauti wameachiwa huru baada ya kupata msaada wa kulipiwa faini zao. Hata hivyo Dkt. Getrude Lwakatale amelipia
gharama ya shilingi milioni 25 ambapo kwa awamu ya kwanza ametoa wafungwa 50 na awamu ya pili itawahusu wafungwa 28. Aidha Lwakatale mara baada ya kutoa msaada huo katika magereza ya Ukonga, Keko, na Segerea amesema kuwa lengo kuu la kutoa msaada huo ni kuisaidia serikali kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani. "Hatutetei uhalifu, msaada huu siyo tu kupunguza wafungwa gerezani bali kurejesha nguvu kazi ya taifa na ndani ya familia kwani wazazi waliofungwa hapa ni masikitiko kwa familia na watoto wao, hivyo tumesaidia familia nyingi kurejesha amani na faraja kwao" Aidha Lwakatale amewaasa wale wote walioachiwa huru kutoka magerezani kuwa wananchi wema wanapoishi na kuacha kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na kujikita katika ujenzi wa taifa,
"Biblia inasema katika Mathayo 25:36-40 kuhusiana kuwaona walioko kifungoni, na mimi kama mtumishi wa Mungu nimeguswa kutimiza andika hilo" amesema Lwakatale amewataka wanaoguswa na tukio hilo kujitokeza kwa wakati mwingine kuwasaidia wale waliofungwa kwa kukosa fedha za faini ili warudi tena uraiani na kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali na maendeleo.
Tanzia:Kocha Wa Zamani Taifa Stars Afariki Dunia
Aliewahi kuwa kocha wa timu ya Taifa Stars na Mwenyekiti wa Makocha Mkoani Morogoro Mohammed Hussein alimaarufu Msomali amefariki dunia jana sababu za kifo chake bado hakijawekwa wazi hadi sasa, Kocha Msomali aliwahi kuzifundisha Taifa Stars na mpaka umauti unamfika alikuwa mwenyekiti wa makocha mkoani Morogoro.
Jumanne, 6 Septemba 2016
Na:Fadhila Kizigo>>>Wales Wafuzu Kombe La Dunia
Hatimaye Wales imefuzu kombe la dunia baada ya michuano ya Euro dhidi ya Moldova mchezo uliochezwa katika uwanja wa Cardiff City Sam Vokes aliifungia goli Wales dakika ya 11 kipindi cha kwanza cha mchezo.Mnamo dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza cha mchezo Joe Allen aliifungia Wales goli la pili. Aidha hadi kumalizika kipindi cha kwanza cha mchezo Moldova walitoka bila kuona lango la Wales Pia mshambuliaji Gareth Bale alifunga magoli mawili kipindi cha pili dakika ya 51 na 91 na mchezo kumalizika kwa matokeo ya goli 4-0 na kuiwezesha Wales kufuzu kombe la dunia.
Jumapili, 4 Septemba 2016
Na:Fadhila Kizigo>> Uhamiaji Waibuka Kidedea Netball Taifa
Hatimaye Uhamiaji washinda michuano ya Netball 2016-2017 ambayo yalikuwa yanafanyika mkoani Morogoro ambapo Uhamiaji waibuka na ushindi huku timu ya Kinondoni ikiburuza mkia. Akizungumza na mwandishi wetu Captain wa timu ya Uhamiaji Jackline Sikozi amesema kuwa ushindi wao unatokana na umahiri wa kucheza kwa ushirikiano uwanjani. Hata hivyo Jackline amesema kuwa kwa ushindi huo ni mwanzo wa mashindano ya Muungano yanayofuatia. Aidha Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh. Annastazia Wambura ametoa wito kwa vyama vya Netball Nchini kuzingatia katiba Pia Wambura ametoa wito kwa wanawake Tanzania kuenzi mchezo wa Netball.
Front Page Za Magazeti Leo Trh 5
Hotel Ya Nyota Tatu Arusha Yapigwa Mnada
Kumekuwa na ongezeko kubwa la Hotel kufungwa nchini huku nyingine zikibadilishwa matumizi na kuwa vyuo, hostel au matumizi mengine. Hali hii imeendelea kuwa mbaya huku hotel kubwa ya kitalii ya Nyota Tatu ya Snow Crest iliyopo jijini Arusha itapigwa mnada tarehe 23/ 9 /2016 ikiwa ni baada ya kesi inayoendeshwa na kati ya bodi ya wadhamini ya NSSF, Hoteli ya Snow Crest na Wildlife Safaris.
Rapa Lil Wayne Atangaza Kustaafu Muziki
Jumamosi, 3 Septemba 2016
Top Stories Katika Magazeti Leo Sept 4
Katika headline za magazeti ya Tanzania leo jumapili tarehe 4 mwezi wa 9 2016 kila gazeti limetoka na angle yake lakini pia kuna Stories kubwa katika Michezo, Siasa, na Hard News.
Na:Fadhila Kizigo>>> Mashindano Ya Netball Taifa Yafana
Kuelekea Fainali ya Netball kitaifa Mkoani Morogoro matokeo ya mechi ambazo zimechezwa
Jeshi-Star Vs TTPL 54-59, CMTU Vs Uhamiaji 22-71, Madini Vs Kinondoni 85-5, Polisi Arusha Vs Jiji Tanga 59=30, Arusha City Vs Ras-Kagera 85-35. Jeshi Star Vs Kinondoni 102-14, CMTU Vs Jiji Tanga 65-33, Polisi Moro Vs Madini 69-14 Polisi Arusha Vs Arusha City 54-43.
Kauli Ya Makonda Baada ya Kuahirisha UKUTA
Ni August 31, 2016 ambapo Chama cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema kilitangaza kuahirisha mikutano, maandamano ya UKUTA kwa mwezi mmoja ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka. Aidha mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amezungumza baada ya chama hicho kuahirisha maandamano ya ukuta 'Maandamano hayajawahi kujenga shule, maandamano hayajawahi kuleta elimu, maandamano hayajawahi kushusha vitu bei maduka bali Maandamano ni Vurugu yaani kuondoka Amani na wale wanaodai demokrasia wanapaswa kwenda kutii tu kanuni zao za Bunge' Kwaiyo kwenye mkoa wetu si tu tarehe 1 basi hakuna mtu kuzurura mahali popote pale, Ukuta ni kiwango cha mwisho cha mtu kufikiri sasa ndio maana wenzetu wameshindwa mwisho wa siku wanatafuta fursa kwa viongozi wa dini kutafuta muafaka' 'Mimi nafikiri naomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania afanye kazi na atekeleze aliyoyasema kipindi cha uchaguzi ili vijana tufanye kazi katika viwanda mbalimbali tuachane na mambo ya UKUTA bali tuangalie vitu vya maendeleo'
Ijumaa, 2 Septemba 2016
Headline Za Magazeti Leo Sept 3
Jumatano, 31 Agosti 2016
Na:Fadhila Kizigo>>Polisi Arusha Waanza Vyema Netball
Timu ya Polisi Arusha ya Netball yaanza vyema michuano ya Netball dhidi ya Tumbaku Morogoro . polisi Arusha imeanza vyema michuano hiyo kwa kuifunga Tumbaku kwa seti 59 kwa 56. Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti kamati ya ufundi kitaifa Asha Sapi amesema kuwa licha ya timu 10 kutoshiriki kati ya 21 nikutokana na uhaba wa kifedha. Aidha Sapi amesema kuwa timu zimeanza vyema kwa kuwa na nidhamu kwa waamuzi.
Na:Fadhila Kizigo>>>Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro Laimarishwa
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limeimarisha viungo kwa kufanya mazoezi maeneo ya manispaa ya Morogoro. Akizungumza na waandishin wa habari kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Matei amesema kuwa mazoezi hayo yamelengwa kwa kuimarisha jeshi na si vinginevyo. Pia kamanda Matei amesema kuwa siku ya kesho wananchi wasiwe na hofu kwani jeshi letu limeimarishwa vyema kwa ulinzi hivyo maandamano hayo ni ya kichochezi hivyo ameomba wananchi kutokuwa na hofu kwani jeshi la polisi limeshakamata wale ambao ni wachochezi na wanaendelea kukamata kwa watakaoleta uchochezi wa maandamano.
Jumanne, 30 Agosti 2016
Na:Fadhila Kizigo>> Mh Kebwe Azindua Mashindano Ya Netball Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Steven Kebwe amezindua Rasmi mashindano ya Netball ligi dalaja la kwanza katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. Mashindano hayo yatakayofanyika viwanja vya Jamhuri mkoani humo yamezinduliwa kwa Mikoa mbalimbali kushiriki michuano hiyo. Hata hivyo Mh.Kebwe ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kuunga mkono suala la michezo kwani lipo kisheria na kufanya hivyo ni kujenga taifa la wanamichezo lakini pia Kebwe ameomba vijana kupambana na Ukimwi ili kujenga nguvu kazi ya Taifa.
Jumatatu, 29 Agosti 2016
>>>Serkali Yaifungia Magic Fm Na Radio 5
Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye ametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi. Hata hivyo Waziri Nape Nnauye amesema huku adhabu hiyo ikianza leo August 29 2016 pia ameiagiza kamati yake kuviita vyombo hivyo kwa ajili ya kuzungumza navyo kisha maamuzi mengine ya kisheria yatachukuliwa.
Jumapili, 28 Agosti 2016
Na:Fadhila Kizigo>>>Genk Wazidi Kung'ara Ubelgiji
Timu anayochezea Mtanzania Mbwana Samatta imezidi kung'ara mara baada ya kuicharanga timu ya Zulte Waregem kwa goli 1-0 katika mchezo wa ligi ya Ubelgiji Zulta Waregem walikubali kichapo hicho wakiwa ugenini (Cristal Arena). Goli lililofungwa na Alejandlo Pozuelo dakika ya 80. Kwa mchezo huo Krc Genk inakamata nafasi ya tatu kati ya 16 kwenye msimamo wa ligi.
Tanzia:Deo Munish Afiwa Na Baba Yake Mzazi
Mlinda mlango nambari moja wa Yanga Deogratius Munish (Dida) amefiwa na baba yake mzazi leo mchana imeelezwa kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kwenye ukurasa wa facebook wa Naipenda Yanga bado chanzo cha kifo cha baba mzazi wa kipa huyo hakijawekwa wazi. Taarifa hiyo inaeleza hivi:"TANZIA..... Uongozi wa Yanga unasikitika kutangaza kifo cha baba yake na mlinda mlaango wetu deogratius munishi 'Dida', baba yake na dida amefariki leo mchana! Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi! Msiba utakuwa mikoroshini.Pumzika kwa amani mzee wetu.POLE SANA DEO MUNISH 'Dida' ". Hata hivyo katika mchezo wa leo Dida amecheza kwa umahiri mkubwa na kuisadia timu yake kupata clean sheet
Jumamosi, 27 Agosti 2016
Mch. Msigwa Atoa Kali Kuhusu Ukuta
Ni kuelekea katika Maandamano yaliyopewa jina la Ukuta yanayoratibiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ambapo yamepamgwa kuanza tarehe 1 ya mwezi wa 9 Aidha mbunge wa Iringa Mjini Mch. Peter Msigwa (Chadema) ametoa kali mara baada ya kuandika katika kurasa yake ya
Twiter kuhusu Maandamano ya Ukuta Mch.Msigwa alisema kuwa "Mwanasiasa wa wa upinzani Tanzania kama anaogopa kukamatwa na Polisi ahamie CCM Huu ndio wakati wa kutofautisha BOYS FROM MEN".
Alhamisi, 25 Agosti 2016
Na.Fadhira Kizigo>>>Stand United Wakanusha Juu Ya Kujitoa VPL
Kufuatia kauli ya Waziri wa Michezo na Utamaduni Mh. Nape Nnauye juu ya sakata la Stand United kujitoa katika ligi ya Vodacom Tanzania bara kumekuwa na sintofahamu kwa mashabiki wa mpira nchini. Akizungumzia suala hilo Mkurugenzi wa benchi la ufundi Stand United Muhibu Kano amemtaka Waziri Nape kuwaomba radhi watanzania kutokana na kitendo cha kutoa kauli hiyo kwan i angeitisha pande zote mbili kuzungumzia hilo na si kwa upande mmoja. Aidha Muhibu amesema amesema suala la kuanza kwa ligi vibaya kwa kutoka sare na Mbao Fc nikutokana na migogoro lakini chanzo cha migogoro ni wachezaji kukosa amani na kutofanya vizuri lakini wamejipanga vyema na mchezo unaofuata jumamosi 27 mwezi huu dhidi ya Kagera Sugar .
Jumatano, 24 Agosti 2016
Na. Fadhira Kizigo>>>>Yanga Out Shirikisho Kwa Point 4
Timu ya Yanga imemaliza michuano ya shirikisho Afrika dhidi ya Tp Mazembe kwa kukubali kipigo cha magori 3 kwa 1 Bolingi wa Tp Mazembe aliifungia timu yake gori la kwanza dakika ya 28, huku kipindi cha pili kuanza dakika 11 Rainford Kalaba aliifungia goli la pili Tp Mazembe kabla ya kuifungia goli la tatu mnamo dakika ya 64 huku goli la kufutia machozi kwa Yanga likiwekwa kimiani na Hamis Tambwe. Lakini kwa upande wa mashabiki wa mpira Mkoani
Morogoro Juma Demele alisema kuwa licha ya kushindwa naipongeza Yanga kwa kufanya vizuri hapo walipofika wana nafasi kwa mwakani kufanya vizuri zaidi hivyo kwa sasa wajipange kufanya vizuri kwa msimu huu wa ligi Tanzania bara pia Mohammed Mnyukwa alisema kuwa viongozi kuwa na ushirikiano na wachezajini jambo la kuzingatiwa kwenye klabu zetu nchini hivyo ni vyema kuwa umoja.
Ijumaa, 12 Agosti 2016
Na:Fadhira kizigo>>>Timu ya Polisi Morogoro Yatangaza kikosi chao
Timu ya polisi Morogoro yatambulisha kikosi chake kitakachoshiriki ligi daraja la kwanza hapo baadae mwezi huu, Afisa habari wa Polisi Morogoro Mwashibanda Shibanda amesema kuwa timu hiyo inamilikiwa na Wananchi na siyo jeshi la polisi hivyo anaomba mashirika mbalimbali kuiwezesha timu hiyo kwa fedha , vifaa,hata mawazo. Kashibanda alitaja orodha ya kikosi cha timu hiyo:walinda mlango. Benjamini Haule, Ramadhani Abedi, na Japhet Mwakyusa, walinzi wa kulia: Shabani Stambuli, Majid Msisis, walinzi wa kushoto: Saimon Samweli, Juma Ramadhani Haji: beki wa kati Omary Mtaki, Abrahaman Bakari, Omary Alawi na Godfrey Francis: viungo wa kati: Salum Bakari Nahodha, Juma Nade, James Ambrose, Bakari Mahadh na Abraham Thomas Bahufashi, winga wa kulia: Bantu Admin, David Christopher, na Hassan Kandabovu, winga wa kushoto: Nicholaus Kabipe, Fadhir Jamali, na Abdallah Maridodi, washambuliaji: Salum Kihimbwa, Ramadhani Kapela, Anyuerisa Mwaipora na Isaya Katua,
Jumamosi, 9 Julai 2016
Whitedent Washeherekea miaka 25 Kwa Kugawa Magari?
Kampuni ya Chemi and cotex industries limited invites washeherekea miaka 25 ya kutumia dawa ya meno aina ya whitedent kampeni hiyo imezinduliwa, na Mkuu wa Wilaya ya Musoma mjini Dr.Vicent Anney. Aidha kampuni hiyo imewashukuru watanzania kwa kutumia dawa ya meno ya whitedent na kwa kuwarudishia shukrani wao kama kampuni wameamua kutoa shindano la gari ambalo magari zaidi 300 yanashindaniwa katika mikoa yote Tanzania. Kwa upande wake Meneja wa kampuni hiyo kwa tawi la mkoa wa Mara Mr. Govind Singh alisema "Kampuni imejipanga kufanya mambo mazuri kwa watumiaji wa bidhaa zao". hata hivyo meneja aliongezea kwa kusema kuwa kila kitu kitaenda vizuri katika kuendesha shindano hilo la kugombania gari aina ya toyota saloon. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Musoma Mjini Dr.Vicent Anney alisema "pamoja na kualikwa katika hafla fupi hiyo amekuwa na tatizo la madawati katika wilaya yake na kuchukua nafasi hiyo kuwaomba kampuni ya Chemi and Cotex kuchangia madawati katika wilaya hiyo kwani kwa kufanya hivyo kutawaamasisha watu kutumia bidhaa zao". Mashindano hayo yanaendelea Nchi nzima kwa watanzania wote kuchukua fomu na kujaza kisha unabashiri viboksi ambavyo vipo kwenye gari kwa kubashiri mara nyingi zaidi baada ya hapo unaweza ukachaguliwa kuingia kwenye droo na ukajishindia gari.
Jumatatu, 4 Julai 2016
Jike Shupa wa Kwenye Tv awa Kiki Mjini
Msanii wa filamu nchini Zena Haji alimaarufu Jike shupa ameingia kwenye headline kwa haraka sana mara baada ya kushirikishwa katika video ya wimbo wa msanii wa bongo Freva Nuhu Mziwanda uitwao Jike shupa. Msanii huyo ambaye alishiriki kama video queen katika wimbo huo ambao unafanya vizuri sana katika media mbalimbali nchini Alisema "Napata matatizo sana kutokana na wimbo huo kwa baadhi ya watu kunifananisha na Shilole". Zena Haji aliongezea kwa kusema kuwa tangu wimbo wa jike shupa umeachiwa hewani amekuwa akipata meseji nyingi sana kutoka kwa mashabiki wake wakimpongeza kwa kufanya vizuri katika wimbo huo pia amekuwa akipata interview nyingi sana katika media mbalimbali kutokana na wimbo huo wa jike shupa. Mwisho alimalizia kwa kusema kuwa wantanzania wasimchukulie kweli kama ana tabia hiyo ila mwisho wa siku ibaki kuwa ni kazi kama kazi nyingine na heshima ibaki kuwa pale pale pia mrembo huyo aliwataka mashabiki wake wakae tayari kwa vitu vizuri kutoka kwake kwani ana matarajio makubwa sana kwa ivi karibuni cha msingi ni mkumuomba mwenyezi Mungu hatufikishe alisema msanii huyo.
DEAL DONE KWA CHELSEA
Klabu ya Chelsea ambayo msimu ujao itaanza kunolewa na aliyekuwa kocha wa wa timu ya taifa ya Italia katika michuano ya Euro 2016 Antonio Conte, imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji aliyekuwa anaichezea Marseille Michy Batshuayi. Michy Batshuayi mwenye umri wa miaka 22 ametangazwa na Chelsea na kusaini mkataba wa miaka mitano ya kuishi ndani ya stamford bridge London England.
Alhamisi, 30 Juni 2016
Kubenea na Joseph Mbilinyi Wasimamishwa kuhudhuria bungeni.
Mbunge wa Ubungo Chadema amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli. Pia Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo june 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili naye achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.
Maguli apata Dili Uarabuni.
Alhamisi, 16 Juni 2016
Fainali Ya Mashindano Ya Kuhifadhi Qur'an tukuf Yaanza Rasmi Jumapili
Assalam aleykum, Aisha Sururu Foundation inayo furaha kuwaalika kwenye fainali ya mashindano ya mwaka 2016 (1437 AH) ya kuhifadhi Qur'an tukufu itakayofanyika jumapili ya tarehe 19/06/2016 katika ukumbi wa Diamond jubilee Hall jijini Dar es salaam, ambapo vijana wanawake na wanaume watakaoshiriki katika mashindano haya watapigania nafasi zao za kwanza kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur'an katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. Mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya mwaka huu yatakuwa ni mashindano ya kumi na nne (14) tangu mashindano ya kuhifadhi Qur'an yanayoandaliwa na Aisha Sururu Foundation yaanzishe, Alhamdulillah. Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 24 ya Tanzania pamoja na visiwa vya Zanzibar, Unguja na Pemba, kwa nia ya kuwashajiisha watoto kuhifadhi Qur'an katika viwango vya juu vya kuisoma Qur'an tukufu. Kauli mbiu ya mwaka huu: Tuwathamini Walimu Wetu wa Qur'an Tukufu, Tupate Radhi za Mola Wetu Ra'ufu.
Jumanne, 14 Juni 2016
Etoo Afunga Ndoa Leo
Ijumaa, 10 Juni 2016
Zoezi La Usajili Vitambulisho Vya Taifa Kukamilika Desemba 31 Mwaka Huu Nchi Nzima
Mamlaka ya usajili wa vitambulisho vya Taifa Nchini Tanzania (NIDA) wametangaza kuwa ifikapo tarehe 31 mwezi 12 mwaka huu usajili wa vitambulisho utakuwa umekamilika nchi nzima. Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es salaam Bi.Rose Mdami, alisema "usajili utakamilika ifikapo tarehe 31 mwezi 12 mwaka huu Nchi zima na wananchi kuanza kutumia namba ya utambulisho kupata huduma" Bi.Rose Mdami ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hatiwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) aliwasisitiza Wananchi wote Nchini kuweza kujiandikisha mapema ili kuepuka usumbufu baadae. Pia Bi. Rose Mdami, amesema NIDA imepanga kutumia taarifa za NEC kukamilisha usajili wa awali na kutoa namba ya utambulisho kwa wananchi wote ambao hawakusajiliwa katika mfumo wa NIDA. Pia akifafanua, Bi.Rose amesema baada ya kuhakikisha kila mwananchi ana nambari ya Utambulisho.kila mwananchi atalazimika kukamilisha usajili wake ikiwa ni hatua ya kujaza vipengele vya maswali vilivyobakia katika fomu ya maombi ya vitambulisho kabla ya kupata utambulisho kamili. "Kama mnavyofahamu, katika usajili wa NEC fomu ilikuwa na vipengele 32 vya kujaza kulinganisha na fomu ya NIDA ambayo ina vipengele 74, hivyo ni lazima kila mwananchi kutambua, ili kuwa na utambulisho kamili lazima kujaza vipengele vilivyobaki pamoja na kuambatanisha nakala ya viambata vyake muhimu kuthibitisha taarifa za umri, uraia na makazi" alilisitiza.
Jumatano, 8 Juni 2016
Tff Yatoa Fomu Za Leseni Kwenye Vilabu
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeanza kutoa fomu za leseni za klabu (Club Licensing) za ligi ya vodacom Tanzania Bara (VPL) na zile za ligi daraja la kwanza ya Star Times. Klabu hizo zitatumiwa fomu hizo na kutakiwa kuzijaza na kuzirejesha kabla ya June 19, mwaka huu ikiwa ni siku 10 mara baada ya Bodi ya Ligi ya TFF (TPLB) kuwatumia fomu hizo. Klabu itakayojaza fomu hizo kwa wakati ndiyo ambayo maombi yake ya leseni yatashughulikiwa mapema. Tayari TFF imeteua kamati ya leseni ya klabu (Club Licensing Committee) ambayo ndiyo yenye jukumu la kupitia maombi ya leseni kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi daraja la Kwanza na kutoa uamuzi wa kuzikubali au kuzikataa kwa kuzingatia Kanuni ya Leseni ya klabu. Wajumbe walioteuliwa kwenye kamati hiyo inayoundwa kwa mara ya kwanza ni wakili Lloyd Nchunga (Mwenyekiti), Wakili Emmanuel Matondo (Makamu Mwenyekiti), David Kivembele, Hamisi Kissiwa na Prof.Mshindo Msolla. Klabu zinatakiwa kuchukua fomu za maombi TFF ambapo baada ya kuzirejesha zitafanyiwa kazi ambapo zile zitakazokuwa zimekidhi matakwa ya Kanuni husika zitapatiwa leseni husika ili zishiriki michuano ya Ligi ya Vodacom na Ligi daraja la Kwanza ya StarTimes kwa msimu wa 2016-2017. Kwa Klabu ambazo zitashindwa kukidhi matakwa ya leseni yanayolenga kuhakikisha mpira wa miguu unaendeshwa kwa weledi na kupiga vita upangaji matokeo katika maeneo matano ya wachezaji (Sporting) viwanja (infrasructure), utawala (administrate and personal), umiliki wa klabu (ownership) na fedha (financial), hazitapata leseni hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki ligi. Klabu ambazo zitanyimwa leseni na kutoridhika na uamuzi huo, z itakuwa na fursa ya kukata rufani kwenye kamati ya Rufani ya Nidhamu ya TFF. Kwa mujibu wa Ibara ya 5(3)ya kanuni ya leseni ya klabu ya TFF, Kamati hiyo ndiyo itakayosikiliza rufani zinazopinga uamuzi wa kamati ya leseni ya TFF.
Alhamisi, 2 Juni 2016
Zengwe Laibuka Upinzani Na Spika Bungeni
June 02 2016 Kambi rasmi ya upinzani bungeni imekutana na waandishi wa habari Dodoma ili kuwasilisha mambo makuu sita imetoa sababu kuu sita za kutaka Naibu spika wa Tanzania Dr.Tulia Ackson aondolewe madarakani kwa azimio la kuvunja sheria inayoendesha bunge. Akiongea kwa niaba ya kambi ya upinzani mbunge wa Simanjiro James Millya amesema "Naibu spika Tulia Ackson ameweka maslahi ya chama chake cha siasa mbele kuliko maslahi ya bunge kinyume na kanuni ya 8 (b) ya kanuni za kudumu za bunge" "kutoa uamuzi wa mwongozo ambao ulikuwa unakiuka katiba isemayo kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake muongozo uliokuwa unapinga udhalilishaji wa wabunge Wanawake UKAWA kwamba hawapati Ubunge mpaka waitwe baby, muongozo ulioombwa Dr.Tulia aliudharau" Tarehe 30 May Naibu spika huyo huyo aliamua kwa makusudi kuvunja ibara ya katiba ya Jamhuli ya muungano wa Tanzania kumzuia Mh. Joshua Nassari kutimiza majukumu yake ya kikatiba ya kusimamia na kuishauri serikali, ni pale alipoomba muongozo wa jambo la dharura la kufukuzwa kwa Wanachuo wa UDOM, Dr. Tulia alisema hoja hiyo sio ya dharura na wala haikuwa na haja yoyoteya kuwasilishwa. Kitendo cha naibu spika Dr. Tulia kukataa taarifa tofauti iliyowasilishwa na Wabunge wanne wa upinzani ambao ni wajumbe wa kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge jambo ambalo ni kinyume cha kanuni ya tano ambapo maamuzi yake haya yalisaidia kuwafukuza wabunge saba wanaolitumikia taifa hili, adhabu iliyotolewa haikuwa adhabu inayostahili.
Jumapili, 29 Mei 2016
TTCL Yazindua Nembo Mpya na 4G LTE
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) yazindua Nembo mpya pamoja na kuzindua huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE Leo jijini Dar es salaam.kampuni hiyo imefanya mabadiliko makubwa ya nembo yake pamoja kuzindua huduma ya mtandao wa kisasa wa 4G LTE ikiwa ni muendelezo wa mpango wa kufanya mabadiliko ya kibiashara kwa kampuni hiyo. Nembo hiyo mpya ya TTCL na huduma ya 4G LTE vimezinduliwa leo jijini Dar es salaam na waziri wa Ujenzi Uchukuzi, na Mawasiliano,ProfesaMakame Mbarawa huku akiipongeza kwa hatua ya kuleta mabadiliko ya kiutendaji na uwajibikaji unaolenga kuonesha tija na ubora. Waziri Mbarawa alisema uzinduzi huo ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli la kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu, na kufikia viwango vya juu kabisa vya kutoa huduma kwa umma sambamba na mpango mkakati wa TTCL, kibiashara kwa kipindi cha mwaka 2016-2018. "Pamoja na pongezi hizi za dhati, naomba mtambue kuwa uzinduzi huu hautakuwa na maana yoyote pasipo mabaliko ya kiutendaji utoaji huduma kwa wateja. Watumiaji wa huduma zenu wanahitaji mabadiliko ya dhati ya viwango vya huduma na utendaji ili kuwajengea imani juu ya uwezo wenu wa kuwahudumia," alisema Waziri Mbarawa, Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk Kamugisha Kazaura alisema uzinduzi wa nemnbo mpya ya TTCL, unaleta muonekano mpya wa kampuni unaoenda sambamba na mageuzi ambayo yanaendelea katika kuboresha miundombinu ya mtandao wa simu data. Alisema katika safari ya mageuzi TTCL imefanikiwa kuboresha miundombinu ya simu za mezani na mkononi kwa kuleta teknolojia ya 2G, GSM, 3G, UMTS, na LTE Sokoni ili kwenda sambamba na ushindani wa soko la mawasiliano. "Teknolojia hizi zitaisaidia kuongeza ufanisi, ubunifu katika kutoa huduma ya simu za mezani, simu za mkononi na huduma ya intaneti zenye ubora wa hali ya juu ya uhakika na gharama nafuu,"alisema Dk. Kazaura. Alisema kwa sasa kampuni hiyo inaendelea na juhudi za kuboresha miundombinu ya mawasiliano ya data nchi nzima, hali ambayo itaongeza ubora wa huduma zetu kwa wateja wetu wote ndani na nje ya nchi.
Ijumaa, 27 Mei 2016
Kivumbi Leo Uefa Champion League
Kuelekea katika Mchezo wa fainali ya League ya Mabingwa barani Ulaya zinazikutanisha Timu mbili kutoka katika jiji moja la Madrid na si wengine ni Atretico Madrid na Real Madrid, Timu ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa katika misimu mitatu mfululizo timu hizo zinazoongozwa na Makocha wawili ambao waliwahi kukupiga katika klabu hizo kipindi cha nyuma nawazungumzia Diego Simeone wa Atretico Madrid na Zinedine Zidane wa Real Madrid. Ikumbukwe kuwa Timu hizi mbili zilikutana kwa mara ya mwisho katika mashindano ya Uefa Champion League mawka 2013 na Real Madrid kuchukua ubingwa,Mchezo wa fainali wa Uefa Champion League utapigwa katika uwanja wa San Siro mjini Milan katika nchi ya Italia mchezo ambao utapigwa majira ya saa 3:45 kwa majira ya saa za Afrika Masharilki, timu hizo leo zimefanya mazoezi ya mwisho kuelekea katika mchezo huo wa fainali. Kocha wa Atretico Madrid Diego Simeone akiwa katika mazungumzo ya mwisho kuelekea mchezo wa kesho, anampongeza kocha wa Real Madrid kwa kufanikisha kusuka upya timu yake na kuifanya kuwa mpya na bora kwa muda mfupi tangu alipoichukua "Zidane amefanya kazi kubwa kukisuka kikosi cha Real Madrid kwa kipindi cha muda mfupi alichokaa na kikosi hicho, amefanya uamuzi mkubwa wa kumuamini na kumpa nafasi kiungo Casemiro, ameifanya timu nzima kuwa imara. Casemiro ndiye mchezaji muhimu kwasasa kwenye kikosi acha Real Madrid",hayo ni maneno ya Diego Simeone wakati anazungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa fainali ya klabu bingwa ulaya. Mshambuliaji wa Atretico Madrid Fernando Torres amesema, kuchukua taji la mabingwa Ulaya akiwa na Atretico itakuwa ni jambo jema licha ya kuwahi kutwaa taji hilo wakati akiwa na klabu ya Chelsea ya England. "Licha ya kushinda mataji kadhaa nikiwa na timu ya taifa ya Hispania pamoja na kutwaa taji la Uefa nikiwa na Chelsea mwaka 2012, nikishinda taji hili nikiwa na Atletico litakuwa muhimu sana kwenye maisha yangu",alisema Fernando Torres ambaye aliifungia Atletico bao pekee kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wakati Barca inaifunga Atletico kwa magoli 2-1 kwenye uwanja wa Camp Nou.
Jumatano, 25 Mei 2016
Twitter kufanyiwa mabadiliko ili kuwavutia watumiaji
Mtandao wa Twitter unafanyiwa marekebisho sheria zake ili kuwarahisishia kazi watumiaji wake na kuufanya uwe wa kuvutia kwa wale wanaojiunga nao kwa mara ya kwanza.Wanachama wa mtandao hao sasa wataweza kuongeza kile wanachochapisha kwenye mtandao huo,zikiwemo picha na video bila ya kuathiri kiwango cha sasa cha maneno 140 ambayo mtu anastahili kuandika. Twiter pia itafanya marekebisho kuhusu jinsi watu wanaweza kuwasiliana katika mtandao.Twiter imekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia, mwanzilishi mwenza wa Twiter na mkurugenzi mkuu Jack Dorsey,aliiambia BBC kuwa lengo lao ni kuhakikisha kuwa wakati watu wanapoutumia unaonekana kuwa ulio na maana. Mdadisi mmoja anasema kuwa hatua hizo zinaashiria mwelekeo mwema, lakini akaongeza kuwa wameangazia suala moja tu ambalo ni kuongeza watumiaji wake. Licha ya mtandao huo kutumiwa sana katika mambo yanayohusu habari mwaka uliopita, umekuwa na wakati mgumu kuwavutia watumiaji wapya suala ambalo linatajwa kuchangiwa na ugumu ulio katika kuutumia. Brian Blau, ambaye ni mchambuzi kutoka shirika la Gartner, anasema matatizo yanaoikumba Twitter kuwapata watumiaji wapya hayawezi kutatuliwa na mabadiliko hayo, Anasema kuwa tatizo kuu ni kuwavutia watumiaji wapya na kuwafanya wawe wazalendo kwa mtandao,Anaendelea kusema kuwa bado Twitter haijalishughulikia hilo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)